Raila Apokelewa kwa Shangwe Kaunti ya Nakuru, Asema Safari ya 2022 Imeanza

July 2024 ยท 2 minute read

Kinara wa ODM Raila Odinga Jumanne Agosti 17 alizuru kaunti ya Nakuru ambapo alipokelewa kwa shangwe.

Wafuasi wa Raila, maarufu kama Baba, walimiminika katika barabara ya Mburu Gichua na Kenyatta Avenu kumpokea Baba.

Licha ya masharti ya kupigana na Covid-19, wafuasi hao walikuwa na kiu cha kumsalimia Baba na hivyo kupuuza agizo la kutotangamana.

Baba alisema alifika Nakuru katika kuendeleza kampeni ya Azimio la Umoja ambayo alisema ni mchakato wa kuwaleta pamoja Wakenya wote.

"Safari ambayo tumeanza leo inanuwia kuunda kivumbi cha kisiasa na falsafa ya umoja ambayo tunahitaji ili kukabili matattizo yanayokabili taifa," alisema Raila.

Pia soma

Nimepata Password Ya Kuingia Mt Kenya, Raila Awaambia Wafuasi Nyanza

Kulingana na viongozi walioandamana na Raila, kambi yake inaunda mrengo ambao utazua kivumbi nchini kwenye uchaguzi wa 2022.

Kuhusu BBI, Raila alisema amejipanga na yuko tyarai kupokea uamuzi wa Mahakama ya Rufaa Ijumaa Agosti 20.

"Tunagonjea mahakama itoe uamuzi Ijumaa kuhusu BBI, wakitoa uamuzi bora ni sawa na wakiamua vingine ni sawa pia. Lakini wajue hakuna mtu anaweza kusimamisha reggae," alisema Raila Odinga.

Raila alisema aliamua kuzindua Azimio la Umoja Nakuru kutokana na umuhimu wake katika siasa za Kenya.

Aidha iliibuka asubuhi kuwa chama cha Jubilee kimeamua kufanya mkataba wa kisiasa na ODM kwa ajili ya siasa za 2022.

"Kutokana na mashauriano ndani ya Jubilee ambayo yalisababisha mkutano wa NMC na uongozi wa bunge, NMC imetoa ruhussa kwa kamati ya chama kufanya mkataba na ODM kuhusu uchaguzi ujao," katibu wa Jubilee Raphael Tuju alisema.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690

Pia soma

DP Ruto Asukumwa Kwenye Kona, Wafuasi Wasubiri Kuona Ujanja Wake

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ394gZhmqZqhnJZ6orzOpJylnaeWeqzDwGaqoZmenMSmecqarKesmWLGonnNmqKuqqVirrSxzJpkrJmWlr%2BqediaZGtoYmd6qrnEmqWzmV6dwa64